Breaking News

RAIS MAGUFULI AELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI YAKE.


 RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa na Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma,  Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali wakishiriki katika dua  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam jana Desemba 17, 2018. (Picha zote na Ikulu).

Na Mwandishi Wetu

RAIS Dk. John Magufuli, ameipongeza BAKWATA na Waislamu wote nchini kwa kuendelea kudumisha amani, umoja, mshikamano na kuyashika vizuri mafunzo ya dini, na amebainisha kuwa mambo hayo yana faida kubwa kwa jamii nzima ya Waislamu na madhehebu mengine.

Dk. Magufuli, alisesema katika kipindi cha miaka 50 taasisi mbalimbali zilizo chini ya BAKWATA na Uislamu kwa ujumla zimeendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji na nyingine na kwamba serikali inatambua mchango huo mkubwa.


RAIS Dk John Magufuli, akimkabidhi Hati ya Heshima Mzee Mohamed Songambele, mmoja wa wazee mashuhuri  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam. 
Aliyasema hayo jana Desemba 17, 2018 alipokuwa akizungumza na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuadhimisha miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo katika ukumbi wa Diamond, Jijini Dar es Salaam.

Magufuli, aliahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake mzuri na BAKWATA na Madhehebu mengine ya Dini, na kutoa wito kwa Waislamu na Waumini wa Madhehebu mengine ya Dini kuendeleza utamaduni mzuri wa kushirikiana, kuvumiliana, kusameheana na kutunza amani, mambo ambayo yanasaidia kuepusha migogoro.

 
RAIS Dk. John  Magufuli akimkabidhi Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry shilingi milioni 30 taslimu wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam jana Desemba  17, 2018

“Naomba niwahakikishie ndugu zangu, Serikali inawapenda Waislamu na inayapenda Madhehebu yote ya Dini, tutaendelea kuhakikisha tunashirikiana kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo la Taifa letu, kwa pamoja tunaweza,” akisema Rais Magufuli.

Aidha, Magufuli alisema juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuharakisha maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege, kuanza mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji, kujenga viwanda, kujenga reli ya kati na kufufua reli ya kaskazini, kujenga meli mpya na kukarabati za zamani, kujenga barabara, kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini, kujenga hospitali na vituo vya afya na kuongeza ukusanyaji wa kodi.
 MAKAMU wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa Kiisalamu kinamama akishiriki katika dua  wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee JANA.Rais huyo alimpongeza Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally kwa uongozi wake mzuri wa BAKWATA, ushirikiano mzuri na taasisi nyingine ikiwemo Serikali na kutojikweza kwake, na pia ametoa mchango wa shilingi Milioni 30 kwa BAKWATA.

Mapema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, alimshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nao katika maadhimisho hayo, amemshukuru kwa kusaidia kujengwa kwa Msikiti mkubwa wa BAKWATA Jijini Dar es Salaam ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 9,000 kwa mara moja, na pia kwa juhudi alizoanza kufuatilia na kurejesha mali za Waislamu zilizoporwa.

MAGUFULI akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond.Rais kwa niaba ya BAKWATA tunakushukuru sana na Waislamu wameridhika sana kwa kuhakikisha msikiti huu unajengwa na ujenzi wake unaendelea vizuri” alisema Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally.
Katika Maadhimisho hayo, Rais Magufuli, pia alikabidhi tuzo kwa Waislamu waliotoa mchango mkubwa katika BAKWATA.

No comments