Breaking News

RAIS MAGUFULI 'AKUNA' MWANG'ONDA *NI KUTOKANA NA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI YAKE.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda, alipomtembela Ikulu Jijini Dar es Salaam jana Desemba 6, 2018. (Picha zote na IKULU).

                      Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, jana Desemba 6, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idaraya Usalama wa Taifa,  Apson Mwang’onda, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo  Mwang’onda, alimshukuru Rais Magufuli, kwa kukubali ombi lake la kumuona na kuzungumza nae na amempongeza kwa uongozi mzuri unaochochea kasi ya maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendelo.
        RAIS Magufuli na Mwang'onda, wakifurahia jambo.

Mwang’onda, aliitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wauzalishaji wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Power Project) na Ujenzi wa madaraja na barabara ambazo, licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

“Mabadiliko ni makubwa sana ambayo yametokea, kuna miradi mikubwa mingi inafanyika sasa hivi, kwa hiyo mabadiliko ni makubwa kusemakweli na yote hayo ni kwamanufaa ya nchi, kwahiyo nachoweza kusema amefanya kazi kubwa kwamaendeleo yanchi,” alisema Mwang’onda.

MAGUFULI,  akifurahia jambo na Mwang’onda, wakati wakiagana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam jana Desemba 6, 2018.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Tano ili itekeleze mipango yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa.

No comments