Breaking News

RAIS MAGUFULI AMLILIA PROFESA MUBOFU.


 
 RAIS  Dk.John Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu,  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) , nyumbani kwa marehemu, Tabata, Dar es Salaam jana Desemba 21.  Mbofu, alifariki dunia Desemba 18, 2018 Nchini Afrika Kusini. (Picha zote na Ikulu).


                                     Mwandishi Wetu

RAIS Dk. John Magufuli ametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Prof. Egid Beatus Mubofu, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM) aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 huko Pretoria, Afrika Kusini.

Rais Magufuli, jana Desemba 21, 2018 alikwenda kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa aarehemu Tabata Jijini Dar es Salaam na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa akiwemo mke wa marehemu Joyce Chamhulo Mubofu, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanafunzi, ndugu, jamaa na marafikii wa marehemu.
MAGUFULI, akimpa pole Joyce Chamhuro, mke wa marehemu Mbofu, pamoja na familiya yake. 

Katika salamu zake, Magufuli alieleze kusikitishwa na kifo cha Prof. Mubofu, ambaye anasema Taifa lilikuwa linamtegemea kutokana na sifa kubwa alizojijengea katika utumishi wake wa umma, ambapo alidhihirisha uchapakazi wa hali ya juu, uadilifu mkubwa, ubunifu, utiifu na kuchukia rushwa.

Kwa mujibu wa Magufuli, alimfahamu Prof. Mubofu tangu akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baadaye akiwa Mhadhiri, na utendaji wake mzuri alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo aliweza kulifanyia mabadiliko, likaongeza tija na kuongeza makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

DK. Magufuli, akizungumza na wafiwa na waombolezaji mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu.

“Prof. Mubofu ametuachia somo kubwa, alikuwa anashika mabilioni ya fedha za Serikali, lakini aliishi maisha ya kawaida, kwa mara nyingine nawapa pole sana wafiwa wote, wahadhiri wa vyuo vikuu mliopo hapa, wanafunzi, ndugu, jamaa na majirani, tumuombee Prof. Mubofu apumzike mahali pema peponi na sisi tuliobaki tuendelee kushikamana pamoja na familia ya marehemu na kuiombea moyo wa subira na uvumilivu,” alisema Rais Magufuli.

No comments