Breaking News

RAIS MAGUFULI ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI WA TAASISI ZA UMMA.


 

                                                   IKULU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ikulu jana Desemba 6, 2018, Magufuli, aliwateua Pius Msekwa, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology – MUST).

Wengine ni  Zakia Meghji, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya  (MUST), Prof. Esnati Chaggu, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Pia, aliwateua Dk. Samwel Gwamaka, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Meja  Jenerali .Mstaafu Michael Isamuhyo, kuwaaMwenyekitiawaaBodiayaaShirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Mwingine ni Profesa. Gaspar  Mhinzi, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo waJuu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, Uteuzi wa viongozi hao umeanza jana  Desemba 6, 2018.

No comments