Breaking News

WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA *ASEMA LITAHAMAMISHA UKUAJI WA UCHUMI NA KUHIFADHI FEDHA ZA WANANCHI. WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wakati alipozindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, leo Desemba 31, 2018.   Kushoto ni mkewe wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. (Pichazote  na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na Mwandishi Wetu, Lindi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amezindua tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.

Kadhalika, Waziri Mkuu alisema ni vizuri kwa Benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
 MAJALIWA, akizindua Tawi la Benki ya CRDB la  Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa,, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim  Ngandirwa.

Majaliwa, aliyasema hayo leo Desemba 31, 2018 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi hilo la Benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao.

Hata hivyo, alisema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo midogo, ya kati na mikubwa  kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi.
KASSIM Majaliwa,  akizindua  Tawi la Benki ya CRDB  la Ruangwa, Desemba 31, 2018.  Wengine pichani kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela

Pia, aliipongeza CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo nchini.

AwaliMkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za fedha.
                                                     JENGO la Benki ya CRDB tawi la Ruangwa. 

Alisema tawi hilo ni la sita katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwani tayari wanamatawi mengine manne ambayo ni Lindi mjini, Mtwara, Masasi, Tandahimba na tawi  linayotembea katika Wilaya ya Newala. Pia wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa tawi Nachingwea.

“Wilaya hii ya Ruangwa ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla, hivyo uwepo wa mfumo rasmi wa kibenki,  kupitia  tawi hili la CRDB, utasaidia sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kufungua fursa mpya,” alisema.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi kompyuta mpakato kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017, Omari  Magoma , baada ya kuzindua tawi la Benki hiyo la Ruangwa. Kompyuta Mpakato 28 zilitolewa na  Benki ya CRDB kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 

Mkurugenzi huyo alisema CRDB wanajivunia utendaji mzuri wa tawi hilo, kwani katika kipindicha mwaka mmoja toka limeanza kazi, limeweza kupata matokeo makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana ambazo zimefikia kiasi cha shilingi bilioni 1.5.
KIONGOZI wa Chama cha Msingi cha Umoja  2017 wilayani Ruangwa, Omari Magoma, akionyesha Kompyuta Mpakato aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  alipozindua tawi la benki hiyo.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
BAADHI ya waarikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa (hayupo pichani).

Tayari jumla ya AMCOS 12 wanachama 4,600 zimejiunga na kufungua akaunti zao hivyo kuongeza usalama wa fedha zao. Pia  jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 1.2 imeshatolewa kwa wateja wa wilaya hiyo, ambapo shilingi milioni 409 zilitolewa katika kilimo cha korosho na ufuta, wakati shilingi milioni 790 zilitolewa kama mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.

No comments