Breaking News

Wizara ya afya yafanya semina kwa waandishi wa habari
Wizara ya afya yafanya semina kwa waandishi wa habari na kuwataka wafikishe elimu sahihi kwa jamii juu ya magonja yasiyopewa kipaumbele na juu ya umuhimu wa kinga tiba juu ya magonjwa hayo.
Magonjwa hayo ni yale ambayo yapo kwenye jamii yetu na dalili zake zinatumia muda mrefu kuonekana au kujitokeza na yana madhara makubwa au kuacha ulemavu kwa jamii. Magonjwa hayo yapo Afrika nzima na mengine Tanzania Zaidi. Mfano wa magonjwa hayo ni USUBI, MATENDE NA MABUSHA(NGIRI MAJI), TRAKOMA, KICHOCHO, MINYOO, MALARIA, KICHAA CHA MBWA, MAGONJWA YA TEGU, TAUNI, FUNZA, KUUMWA NA NYOKA, UKOMA & MAGONJWA YANAYOTOKANA NA CHAWA. Baadhi ya magonjwa hayo shirika la afya Duniani limeyaundia mpango wa kuyatibu na kuyatokomeza kwa kutumia mkakati wa tiba kinga. Upo toaji wa dawa unafanyika kwa ajili ya tiba na kinga, hata kama hujaathirika ni muhimu kunywa dawa kwa ajili ya kujitengenezea kinga na kuondoka kwenye hali hatarishi ya kupata hayo magonjwa. Hayo yamesemwa na DR. Upendo John ambae ni mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

No comments