Breaking News

BOSS KAMPUNI YA AIRTEL ANYOSHA MIKONO KWA JPM. 
 RAIS Dk. John Magufuli, akisalimiana na mgeni wake Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) Sunil Mittal, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo , Ikulu Jijini Dar es Salaam. Leo Januari 11,2019. (Picha zote na Ikulu).                               
                                       Na Mwandishi Wetu

RaiswaJamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Januari, 2019 amekutana na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Bw. Sunil Mittal, Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumzia maendeleo ya mazungumzo ya umiliki wa hisa za kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  Tanzania.

MWENYEKITI wa Kampuni ya Bharti Airtel, Sunil Mittal amesema kampuni yake imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania katika Kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi 49, hivyo kupunguza hisa zilizokuwa zikimilikiwa na Bharti Airtel kutoka asilimia 60 hadiasilimia 51.


DK. John Magufuli, akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mittal aliyeambatana na ujumbe wake kutoka Kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC ) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu.


Aliyasema hayo leo Januari 11, 2019 katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dk. John Magufuli yaliyofanyika  Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumzia maendeleo ya mazungumzo ya umiliki wa hisa za Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  Tanzania.


Mittal, alisema kuwa, mazungumzo kati ya kampuni yake na Serikali ya Tanzania yanakwenda vizuri na kwamba Kampuni ya Bharti Airtel imeridhishwa na makubaliano yaliyofikiwa katika masuala yaliyokuwa ya kijadiliwa yenye lengo la kuiimarisha kampuni ya Airtel kuleta manufaa kwa pande zote mbili na kuboresha huduma za mawasiliano za kampunihiyo.

 RAIS Dk.  Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Mittal  mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam.Kwa upande wake Rais Dk. Magufuli, alielezea kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo ambapo pamoja na kuongeza hisa za Serikali katika umilikiwa Airtel Tanzania, kampuni hiyo imekubali kutoa gawio kwa Serikali ya Tanzania mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika hivi karibuni.

“Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo haya yataendelea leo ili kumalizia, lakini jambo zuri nikuwa sasa wamekubali kutoa gawio kwa Serikali ambapo kwa muda wa miaka minane hadi kumi tulikuwa hatujalipata.

“Kiasi cha asilimia za gawio nacho watajadili leo, kwahiyo mimi naona huu ni mwanga mzuri wa kwenda mbele kati ya kampuni ya Bharti Airtel na Serikaliya Tanzania pamoja na kampuni zingine,” alisema Rais Magufuli.
RAIS Dk. Magufuli, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bharti Airtel Sunil Mittal, aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu, Mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Ikulu Jijini Dar es Salaam.Kwa upande wa Tanzania timu ya majadiliano na Kampuni ya Bharti Airtel inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.

No comments