Breaking News

KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU AKABIDHIWA OFISI.

 KATIBU Mkuu mpya  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),  Dorothy Mwaluko, akikabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Profesa, Faustin Kamuzora, ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu  Tawala  mkoani Kagera. Kabla ya uteuzi huo, Dorothy  alikuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejineti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Januari 16, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu). KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi, akishuhudia makabidhiano rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Katibu Mkuu mpya  Dorothy kutoka kwa  Kamuzora.

 PROFESA. Faustin Kamuzora, akishukuru kwa ushirikiano aliokuwa anapewa wakati  akihudumu katika ofisi hiyo, kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna (katikati) na Dorothy.

 KAMUZORA, akiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa  Makatibu Muhtasi wake,  pamoja na Katibu Mkuu mpya  Dorothy (kulia), mara baada ya kumkabidhi ofisi.


KATIBU Mkuu mpya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Dorothy.

No comments