Breaking News

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO GHOROFA MBILI LA KITUO CHA MAMA NA MTOTO KMKM KIBWENI ZANZIBAR. 
JENGO la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni, wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini Magharibi, Unguja ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Samia Suluhu Hassan, ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 

                         Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan,  amewataka wanaotoa huduma katika Sekta ya Afya kuhakikisha inakuwa bora.

Samia, alitoa rai hiyo leo Januari 7, 2019, wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Afya cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 SAMIA, akisalimiana na Mkuu wa KMKM Komodoo Hassan Mussa Mzee, wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni.

Aliwataka  Wataalamu wa Afya Nchini kutambua kuwa wanatakiwa  kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara.

“Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini,” alisema Makamu wa Rais.

 SAMIA akisalimiana na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ali Karume.

Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto lina ukubwa wa ghorofa mbili na limegharimu jumla ya sh. Bilioni  3, 648,400,000/- na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Huduma  zitakazotolewa   kwenye  kitu hicho cha afya  ni ya  Mama na Mtoto, Wodi ya Wazazi na Watoto, Upasuaji kwa Mama Wajawazito, Vipimo X Ray, Utra Sound na Maabara, Ofisi za huduma za madaktari, wauguzi na wahudumu wengineo.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongezi mara baada ya kukata utepe kuashiri uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir (kulia) na kushoto ni Mkuu wa KMKM Komodoo Hassan Mussa Mzee.

Mradi huo wa ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ni utekelezaji kwa vitendo wa malengo halisi ya mwasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ambaye alidhamiria kuimarisha huduma ya afya kwa wakulima.
    MOJA ya chumba cha kutoa huduma ya Afya katika jengo hilo.

Uzinduzi wa Jengo hilo umerahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa maeneo ya Kibweni, Mwanyanya, Bububu, Mbuzini, Mtoni, Kama, Mfenesini, Mahonda, Mtopepo na maeneo mengine.


                        MAKAMU wa Rais Samia akikagua jengo hilo.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu  za SMZ  Haji Omar Kheir alisema Serikali itaendelea kusimamia yale yanayopaswa kutekelezwa haswa kwenye huduma za afya.

No comments