Breaking News

MBUNGE AYSHAROSE ABORESHA MIUNDOMBINU SHULE YA MWANKOKO.                           
                                 Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,  ameendeleza kasi yake ya kuhakikisha miundombinu ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa, maabara na vyoo vinaboreshwa ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu.

 Aysharose, alianza kampeni yake hiyo ya kuboresha miundombinu katika shule mbalimbali za mkoa wa Singida baada ya kukutana na changamoto za miundo mbinu isiyo rafiki kwa wanafunzi, wakati akiwa kwenye ziara zake za kikazi.
Juzi, Aysharose, alikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji katika shule ya Sekondari Mwankoko kwa ajili ya kuboresha miundombinu shuleni hapo. Msaada huo ulikabidhiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu,  kwa niaba ya mbunge huyo.

Katika hafla hiyo, Yagi alisema kuwa dhamira ya mbunge huyo  ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira bora ili kusaidia kuongeza ufaulu.
"Aysharose ana dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha wanafunzi ambao ni watoto wetu wanasoma vizuri. Kukiwa na madarasa mazuri watoto wetu wanakuwa kwenye mazingira bora ya kujifunza na  tunawaepusha na mambo mengi ambayo yanaweza kuwa kikwazo kwao katika kutimiza malengo.
Alisema msaada kama huu haujatolewa  hapa Mwankoko tu bali kwenye shule mbalimbali za mkoa wetu wa Singida, lengo ni kuona shule zinapofunguliwa basi watoto wetu wanakuta mazingira mazuri ya kujifunzia.

No comments