WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMILISHWA KWA KANUNI ZA MASOKO YA MADINI
*Ataka maagizo ya Rais
kuhusu masoko ya madini yatekelezwe haraka
WAKUU wa mikoa
wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia
kwenye ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
BAADHI ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Majaliwa.
MAJALIWA akiwahutubia wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara.
WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Madini Dotto Biteko, wakati akiwasili
kwenye ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma jana Januari 26, 2019, kufungua mkutano
wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara.
----------------------------
Na Khadija Mussa, Dodoma
Na Khadija Mussa, Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameuagiza uongozi wa Wizara
ya Madini uhakikishe kanuni za uendeshaji wa masoko ya madini katika mikoa yote
nchini zinakamilika na kuanza kutumika kwa wakati ili kuongeza tija kwenye
sekta hiyo.
Kauli hiyo ya Majaliwa, imekuja siku chache baada ya hivi
karibuni, akizungumzia kuhusu changamoto ya kukabiliana na utoroshwaji wa
madini nchini, Rais Dk. John Magufuli, aliagiza kuanzishwa kwa masoko ya madini
kwenye mikoa yote.
Kutokana na agizo hilo, Waziri Mkuu aliitaka Wizara ya
Madini na wakuu wote wa mikoa watekeleze agizo hilo la haraka iwezekanavyo.
Majaliwa, alieyasema hayo jana Januari 26, 2019 wakati
akifungua mkutano kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini katika mikoa yote
nchini.
Mkutano huo wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa
mikoa, ulifanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dodoma na kuhudhuriwa na mawaziri,
manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu, watendaji wa Wizara
ya Madini pamoja na wa Tume ya Madini.
Waziri Mkuu alisema katika kuanzishwa kwa masoko hayo,
rasimu ya kanuni imeandaliwa na hivyo ni vema wakazielewa vizuri kwa sababu wao
ndiyo watakaozitekeleza kwenye maeneo yao ili Serikali iweze kufikia lengo
ililojiwekea katika kuimarisha sekta ya madini.
”Kutokana na umuhimu wa masoko hayo naagiza kanuni hizo
zikamilishwe haraka iwezekanavyo ili kuwasaidia watu wetu kupata masoko ya
uhakika ya madini na Serikali itanufaika na mrabaha na tozo mbalimbali
zitakazokuwa zikitozwa kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Kadhalika, Waziri Mkuu aliagiza pindi kanuni hizo
zitakapokamilika, Wizara ya Madini ihakikishe zinafikishwa kwa wakurugenzi wa
majiji, manispaa na halmashauri za wilaya, maeneo ya machimbo, wachimbaji na
wafanyabiashara wa madini ili kuondoa migogoro.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliongeza kuwa OR-TAMISEMI
kupitia wakuu wa mikoa na maofisa tawala wa mikoa wakishirikiana na Wizara na
Tume ya Madini waandae taratibu zitakazowezesha Wakurugenzi wa halmashauri
kutoa maoni katika kuanzisha masoko.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka
wakuu wa mikoa wakasimamie kikamilifu masuala ya ulinzi na usalama kwenye
masoko hayo ili kuwahakikishia wafanyabiashara, wachimbaji na wananchi usalama
wa kutosha wakati wa kuuza madini hayo.
Alisema kwa muda mrefu Rais Dk. Magufuli, amekuwa akisisitiza
kuhusu sekta ya madini kuchangia ipasavyo katika pato la Taifa na hivyo kuleta
maendeleo ya kiuchumi na kijami kwa wananchi, lakini sekta hiyo imekuwa na
matatizo ikiwemo utoroshwaji wa madini na migogoro kwa wachimbaji hususani
wachimbaji wadogo.
”Jitihada mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha
changamoto hizo zinaondolewa kwa lengo la kuongeza tija kwenye sekta ya madini..apenda
mfahamu kuwa mna nafasi muhimu katika kuifanya sekta hii iweze kuleta manufaa
yanayotarajiwa kwa Taifa,” alisema Majaliwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Doto Biteko alisema
mkutano muhimu kwa sababu linalenga kumaliza changamoto ya masoko ya madini
nchini, hivyo amewataka wakuu wa mikoa wahakikisha walipa kipaumbele jambo hilo
kwa kuwa linamanufaa kwa Taifa.
Alisema kwa sasa
wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hawana maeneo maalum wanayoweza
kufanyia biashara ya madini hali ambayo inachangia kuwepo kwa
utoroshwaji wa madini, jambo ambalo linasababisha Serikali kukosa mapato.
Waziri Biteko ameongeza
kuwa ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya madini, Wizara iliunda
kamati iliyojumuisha wajumbe kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali
zikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na
Biashara, Benki Kuu na Tume ya Madini.
Alisema kamati hiyo
iliundwa ili kuandaa rasimu ya Kanuni za kuanzisha na kusimamia Masoko ya
Madini Nchini. “Katika kuandaa kanuni hizo, jina la kanuni linapondekezwa liwe
The Mining (Mineral and Gem House) Regulations, 2019," aliesema Waziri
Biteko.
WAZIRI Mkuu akisalimiana
na Mkuu (kushoto), wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, wakati akiwasili kwenye
mkutano wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara, katika
ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma jana Januari 26, 2019. Katikati ni Waziri wa
Madini, Dotto Biteko.
BAADHI ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Majaliwa.
MAJALIWA akiwahutubia wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara.
WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole
Sendeka, mara baada ya kufungua mkutano huo. Katikati ni Waziri Dotto Biteko.
NAIBU Waziri wa
Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (kulia), akimsikiliza Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, katika ukumbi huo. Kutoka kushoto ni Wakuu wa Mkoa ya Iringa
Ally Hapi na Njombe Christopher Ole Sendeka.
MAJALIWA (kushoto) akimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, mara baada ya kufungua mkutano huo. (Picha zote na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
No comments