Breaking News

RAIS DK MAGUFULI AFANYA UTEUZI, LEO

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka yaUvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, MifugonaUvuvi - Zanzibar.

Wakatihuohuo, Mhe. Rais Magufulia memteua Dkt. Emmanuel  Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Uteuzi wa Dkt. Sweke umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Livestock Research Institute - TAFIRI) – Kigoma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).

Uteuziwa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.

Hali kadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia naUtafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania - GST).

Uteuzi wa Prof. Ikingura umeanza tarehe 18 Januari, 2019.

Gerson Msigwa

MkurugenziwaMawasilianoyaRais, IKULU

Dar es Salaam

30 Januari, 2019

No comments