Breaking News

RAIS DK.. MAGUFULI NA MKEWE JANETH MAGUFULI WAMJULIA HALI WAIZRI MKUU MSTAAFU DK. SALIM AHMED SALIM ANAYEPATIWA MATIBABU JIJINI DAR ES SALAAM.

RAIS Dk. John Magufuli, akimjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim, hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli, leo Januari 2 ,2019. (Picha zote na Ikulu).

                        Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, leo Januari 2, 2019 amemjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam baada ya kufanyiwa upasuaji.
DK. John Magufuli, Mama Janeth Magufuli na Mama Amne Salim (mke wa Dk. .Salim), wakimuombea dua maalumu Waziri Mkuu Mstaafu,  Dk. Salim Ahmed Salim, walipomtembelea hopitalini Jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

Pamoja na kutoa pole kwa Dk. Salim, Magufuli. akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, aliongoza sala ya kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili apone haraka.

Dk. Salim alilazwa hospitalini jana Januari 1, 2019 na hali yake inaendelea vizuri.

No comments