Breaking News

SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR.

 
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, jana Januari 10,  2019 . Mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,  Mohamed Aboud. (Picha zote na Ofisi wa Makamu wa Rais).

  MSANIFU wa Majengo kutoka Ofisi ya Wakala wa Majengo,  Hawa Natepe akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kuwekwa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais. Zanzibar  katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
 SAMIA akihutubia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi. 
 MCHORO wa nyumba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ambayo inajengwa Pagali Shehia ya Mkoroshini, Chake Chake Pemba ambapo jiwe la msingi wa ujenzi wa makazi hayo limewekwa na Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,  ikiwa  ni sehemu ya shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar.WASANII wa ngoma za asili wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma ya Kilumbizi yenye asili ya Pujini wilaya ya Chake Chake Pemba wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi.

No comments