Breaking News

WADAU WA SEKTA YA UVUVI WATAKIWA KUTOA MAONI YA RASIMU ZA SHERIA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. LUHAGA JOELSON MPINA (Mb), anakaribisha wadau wa Sekta ya Uvuvi, kutoa maoni kuhusu rasimu za Sheria za Uvuvi na Sheria mpya ya Ukuzaji Viumbe Maji.
RASIMU hizo zinapatikana kwenye tovuti: www.mifugouvuvi.go.tz
TOA maoni kupitia barua pepe maalum ambayo ni; maoni@uvuvi.go.tz
Lengo kuu la kupokea maoni ni kuwashirikisha wadau
katika kuboresha Sekta ya Uvuvi nchini.
Tafadhali tunaomba ushirikiano wako katika kuufahamisha umma ili uweze kushiriki katika maoni haya muhimu kwa Sekta ya Uvuvi.

Imetolewa: Kitengo cha MAwasiliano Serikalini
                     Wizara ya Mifugo na Uvuvi
                     29.01.2019

No comments