Breaking News

WATUMISHI WENZANGU NIPENI USHIRIKIANO TUCHAPE KAZI-DK. MICHAEL.

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Francis Michael, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Peter Mabale, mara baada ya kuripoti  ofisini kwake  Jijini  Dodoma leo Januari 14, 2019 kuanza kazi rasmi.Na Happy Shayo, Dodoma
 
NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Francis Michael, ameomba kupewa ushirikiano na watumishi wa ofisi yake ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wadau na wananchi.

Dk. Michael, alisema hayo leo Januari 14, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.


DK. Francis Michael, akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti ofisini kwake.


Alisema, watumishi wa ofisi yake wana uelewa mkubwa kuhusiana na masuala ya kiutumishi, hivyo, ushirikiano atakaoupata utamsaidia kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutimiza malengo ya Rais Dk. John Magufuli, ya kuwahudumia wananchi.
Aidha, Dk. Michael, ameipongeza Menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia watumishi wa umma nchini.
KAIMU Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Donald Bombo, akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Francis Michael, kwa Menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, kabla ya Michael, kuzungumza na menejimenti hiyo


Aliongeza kuwa, kazi ya kuwahudumia watumishi ni ngumu sana lakini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekuwa ikifanya vizuri sana na hii imejidhihirisha pale alipopata huduma inayostahili kupitia wawakilishi aliokuwa akiwaagiza mara kwa mara.
Pia, aliitaka menejimenti ya ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwake kama ilivyokuwa ikifanya kwa Naibu Katibu Mkuu aliyepita ili kufikia malengo ya Rais.
 DK. Michael, akizungumza na Menejimenti ya ofisi yake. (haipo pichani).


Naye, Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Priscus Kiwango, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, aliahidi kutoa ushirikiano mzuri na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi.
Rais Magufuli, alimteua Dk. Francis Michael, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Januari 8, 2019 na kumuapisha Januari 9, 2019.

                               NAIBU Katibu Mkuu Dk. Michael.
Dk. Michael, amechukua nafasi ya Dorothy Mwaluko, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji).

No comments