Breaking News

WAZIRI JENISTA AKERWA NA SEKTA BINAFSI YA ULINZI KUONGOZA KWA MIGOGORO MAHALI PA KAZI.


 WAZIRI wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu),  Jenista Mhagama  akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la  Wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hawapo pichani) kilichowakutanisha Wasuluhishi na  Waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro, leo Januari 14,  2019.

                        Na Mwandishi Wetu, MorogoroWAZIRI wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, kuweka mpango Maalumu wa kuhakikisha migogoro   katika sekta  binafsi ya ulinzi inapungua. 


MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu akizungumza wakati wa kikao hicho.Alisema, kuwepo kwa wingi kwa migogoro hiyo, kuna sababisha kutumika vibaya kwa rasilimali pindi mwajiri na mfanyakazi wanapogonga kimaslahi na hivyo kuchelewesha maendeleo.   
        

Waziri Jenista, alibainisha kuwa sekta  nyingine zinazoongoza kuwa na migogoro mahala pa kazi ni  Ujenzi na  Elimu na  ameitaka tume hiyo kufanya utafiti kwa sekta   zote zinazoongoza kwa migogoro ya kikazi ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo na kuandaa mkakati maalumu wa kuishughulikia.

Waziri Jenista aliyasema leo Januari 14, 2019 mjini Morogoro   wakati wa kikao cha Baraza la  Wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  Waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima.  
  BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la  Wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wakiwa katika kikao hicho."Hii sekta  binafsi ya ulinzi kwa nini huko migogoro  haiishi?. Nataka mpango wa kumaliza migogoro hiyo, shirikianane na taasisi nyingine muweke mpango maalum utakao weza kutatua na kuhakikisha haizalishwi mogogoro  mingin,e" alisisitiza Janista.

Alifafanua kuwa Serikali ya Awam  ya Tano  inayoogozwa na  Rais Dk. John Magufuli, imedhamiria kwa vitendo  kupiga vita uzembe, ubadhirifu na rushwa mahala  pa kazi.  

 MMOJA wa  Wajumbe wa Baraza la  Wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi akichangia hoja  katika kikao hicho. "Nisisitize kazi ya usuluhishi na uamuzi ni  kazi ya heshima na pia ni  kazi ya wito. Hivyo wekeni mkazo kwenye suala la Usuluhishi ili kupunguza muda  na mlundikano wa  mashauri, pia bainisheni sekta  nyingine zenye migogoro  mikubwa.

“Elimu ni  vyema iendelee kutolewa kwa wadau kuhusu sheria za ajira na mahusiano kazini," aliselema.
  
Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu, alibainisha kuwa tume hiyo itatekeleza maagizo hayo kwa kuboresha mkakati wa mpango kazi wa tume ili kuwa na mpango mkakati kwenye mtazamo wa kupunguza migogoro  na unaolenga kumaliza migogoro kwa nataka katika sekta  zinazoongoza kuwa na migogoro mahala  pa kazi.

 WAZIRI wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu),  Jenista Mhagama,  akiwa katikapicha ya pamoja na Wajumbe wa  kikao cha Baraza la  Wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro. "Tumekuwa tunajitahidi kumaliza na kuipunguza migogoro ya kikazi, kwani tumefanikiwa kumaliza migogoro hiyo kwa asilimia 80 kwenye hatua ya Uamuzi na asilimia 77, kwenye hatua ya Usuluhishi" alisema Nungu.       
             
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi  ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo  kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo kimefanyika kwa mujibu wa agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970. Baraza hilo   huiwezesha tume kuboresha huduma na masuala ya utatuzi wa migogoro ya kikazi kwa njia ya usuluhishi na uamuzi.

No comments