Breaking News

HAPA KAZI TU., SERIKALI YAENDELEA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi mara baada ya kuwasili Igunga, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.

MAKAMU WA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za  Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .
Lengo la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika katika ziara. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili Igunga mkoani Tabora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments