Breaking News

MAGUFULI ATENGUA NA KUTEUA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF


Rais wa JamhuriyaMuunganowa Tanzania, John Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund - PSSSF).

Bw. Kashimba anachukua nafasi ya Bw.Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.
Wakatihuohuo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine kamaifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa  Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).

Na pili, Rais Magufuli amemteua Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.

No comments