Breaking News

MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MAJI WA MUHANGE WILAYANI KAKONKO. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Maji wa  Muhange wilayani Kakonko kukagua mradi huo, Februari 19, 2019. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mbunge wa Buyungu, Mhandishi Christopher Chiza. 

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha  Muhange wilayani Kakonko.

 Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, Februari 19, 2019.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga, Mbunge wa Buyungu Christopher Chiza, Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Joyce Ndalichako na kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhange wilayani Kakonko, Ibrahim Katunzi jumla ya shilingi milioni moja kwa ajili ya Mradi wa Maji na Zahanati katika Kata hiyo, Februari  19, 2019. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments