Breaking News

MKUCHIKA AWATOA HOFU WATUMISHI, AWATAKA WAWE NA SUBIRA JUU YA NYONGEZA YA MISHAHARA.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa watumishi wa umma wa kufanya kazi kwa bidii katika kuleta maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George  Mkuchika wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Amesema,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli anatambua na kuridhika na uwajibikaji wa watumishi wa umma ulioiwezesha Tanzania kufanikiwa katika ujenzi wa miundombinu, kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya serikali na pia kutoa huduma bora kwawananchi.
 Ameainisha kuwa, utendaji mzuri wa watumishi wa umma umeifanya serikali kuwafurahisha watumishi hao kwa kuwalipa mshahara mapema zaidi kabla ya mwisho wa mwezi tofauti na zamani ambapo mshahara ulitoka baada ya mwezi husika kupita.
 Amewaomba watumishi wa umma kuwa na subira kuhusu nyongeza ya mshahara kwa sababu kwasasa serikali imeweka vipaumbele katika kutimiza malengo yake yakiwemo ya ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa usafiri wa anga na ununuzi wa boti kwenye maziwa makuu.
Aidha, amesema kuwa, kuna baadhi ya watumishi waumma wachache wanao haribu sifa ya utumishi wa umma na kusisitiza kuwa mtumishi yeyote anaye haribu sifa ya utumishi atachukuliwa hatua za kinidhamu ilikulinda hadhi ya utumishi wa umma.
 Mkuchika yuko katika ziara ya kikazi mkoani Lindi yenye lengo la   kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo ambapo hadi sasa amesha tembelea Wilaya ya Liwale, Nachingwea Ruangwa na ManispaayaLindi. 

No comments