Breaking News

MPINA ATOA MAAGIZO MAZITO YA UHIMILISHAJI NA UHAMILISHAJI MIFUGO NCHINI

                                WAZIRI LUHAGA MPINA

                               Na John Mapepele, Mpwapwa

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, amemuagiza Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani kuandaa haraka kanuni na mwongozo utakaosimamia kuanzia uvunaji wa mbegu, uuzaji, usambazaji na uhimilishaji na uhamilisha mifugo kabla ya mwezi Machi mwaka huu ili kuwadhibiti madalali wote wanaokwenda kuwaumiza wananchi kwa kutumia kivuli cha Serikali.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mradi wa uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya viinitete na uhawilishaji (MOET) unaotekelezwa na Taasisiya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kituo cha Mpwampwa mkoani Dodoma, Waziri Mpina alisema Watanzania wajivunie mradi huo ambao ni wa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Alisema kupatikana kwa teknolojia ya MOET kumeiwezesha Tanzania kuwa na njiatatu za kuboresha Koosafu ya mifugo ambapo ni njia ya asili ya kutumia madume bora, uhimilishaji (AI) na Uhamilishaji (MOET) ambapo itachochea mageuzi makubwa ya uboreshaji wa koosafu ya mifugo ambayo itaongeza uzalishaji wa maziwa,  nyama,  ngozi na mazao mengine ya mifugo.

Aidha, aliagiza kuwa kila ifikapo mwezi Machi ya kila mwaka idara yake iwe imepeleka ajenda za kufanyiwa utafiti kwenye Taasisi ya Utafiti wa Mifugo ili kupata matokeo ya tafiti ambazo Watanzania wana umiza vichwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayow akabili na kuweka utaratibu wa kupokea tafiti kutoka nje ya nchi.

Pia, amemwagiza Mkurugenzi huyo wa Utafiti, Mafunzo na Ugani kukutana na wazalishaji wa mayai, vifaranga, ng’ombe, kuku,  mbuzi,  kondoo,  punda, nguruwe, viwandavyanyama, ngozi na maziwa ili kujua mahitaji yao kwa sasa ni yepi kwani wao ndio wataotengeneza ajenda  za utafiti zenye uhitaji kwa sasa.

Amekosoa mfumo wa uendeshaji wa tafiti za mifugo nchini kwa kutokuwa na ajenda mahusus I zinazohitajika kufanyiwa tafiti badala yake watafiti wengi wamekuwa wakiendesha tafiti za biashara kwa mataifa mengine ambazo hazina msaada kwa Watanzania.

Amesema mfumo wa kuibua  ajenda za utafiti haufahamiki huku kukiwa na ushirikishwa ji dhaifu wa wadau hali inayosababisha tafiti nyingi kushindwa kutoa majawabu ya matatizo katika sekta ya mifugo nchini huku matokeo na mazao yatafiti hizo yakiwafikia watu wa chache kinyume na malengo ya Serikali.

 Waziri Mpina alisema pamoja  na kuwepo kwa njia zote hizo za uboreshaji Koosafu za mifugo bado kuna kasoro nyingi katika utaratibu unaotumika kuzalisha, kununua, kusambaza na kupandisha mifugo hali inayopelekea zoezi kuwa la kusuasua.

Alisema pamoja na mbegu hizo kuzalishwa na Serikali na kuuzwa mrija mmoja kwa sh. 3,000 lakini kutokana na kutokuwepo mfumo madhubuti wa usimamizi na kuachiwawafanyabiashara binafsi kwenda kuwauzia wafugaji kati ya sh. 20,000 hadish 60,000 kwa mrija jambo linawakatisha tamaa  wafugaji na kutofikiwa malengoyaSerikali.
    
Hivyo Waziri Mpinaalisemajuhudizotezinazofanywa na Serikali za kuzalishambegu bora katikavituovyakevya NAIC Arusha na TaliriMpwapwahaitakuwa na maanakamakasorozilizoposasahazitaondolewa.

Kwa upande wake Mkurungezi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Angello Mwilawa alimhakikishia Waziri Mpina kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wamaagizo yake ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na jitihada hizo zinazofanywa na Serikali ya awamuya tano katika mkakati wake wa uboreshaji wa koosafu ya mifugo nchini.

Naye Mkurungezi Mkuu wa  TARILI, Dk.  Eligy Shirima alisema mradi huo wa MOET unafadhili na COSTECH kwa gharama ya sh. Milioni 400 kwa ajili ya kununua vifaa vitakavyo wezesha kukamua mbegu za dume na kuziweka kwenye jike maalumu lililoandaliwa.

Dk. Shirima alisema jike hilo baada ya kuwekewa hormones husaidia mayai mengi kuiva kwa mara moja na kurutubishwa ambapo mbeguz ilizorutubishwa hunyonywa  na kuhifadhiwa na kasha kusambazwa kwa wafugaji kwa ajili ya uhamilishaji hatuaa mbayo itawezesha kupatika na mifugo bora.

No comments