Breaking News

PICHA: ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KALIUA


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya kutengeneza sabuni bora kutoka kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Wazalendo Imani Matabula wakati wa maonyesho ya wajasiriamali katika viwanja vya Kolimba wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kaliua na Waziri wa Zamani katika Wizara mbali mbali Juma Kapuya(kushoto) mara baada ya kumaliza kuhutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara (kushoto) kabla ya kuhutubia  mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments