Breaking News

PICHA: ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI MKALAMA


 Muonekano wa daraja la Sibiti ambalo kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) walizozitoa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu ambapo wamesema ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 94.8%.

 Naibu Waziri wa Maji Juma Awesu akimsalimia Lailat Ramadhani mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Iguguno wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu  mkoani Singida.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Sibiti kutoka kwa Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Singida Matari J. Masige (kushoto) ambalo limekamilika kwa asilimia 94.8%,kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. 

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso akijibu hoja za wananchi wa Ibaga (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibaga wilaya ya Mkalama ambao waliusimamisha msafara wake kwa lengo la kumsalimu ,Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments