Breaking News

PICHA: ZIARA YA MARY MWANJELWA KISALAWE
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe.

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Naibu Waziri, Mary Mwanjelwa (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya Naibu Waziri huyo  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe.

Naibu Waziri,  Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Mary Mwanjelwa  akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo.

Naibu Waziri Mary Mwanjelwa akishuhudia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. Aliyeambatana naye ni  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.


No comments