Breaking News

PICHA:WAZIRI WA NISHATI, MEDARD KALEMANI AKIWA KWENYE ZIARA YA UWASHAJI UMEME VIJIJINI.Waziri wa Nishati, Medard Kalemani, akiwasha umeme katika Kata ya Kanyala wilayani Geita ambayo imepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III).

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, (katikati) akiwasha umeme katika Kijiji  cha Lwezera wilayani Geita ambacho kimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III).Kushoto kwake ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Amos Maganga.
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani ( wa Tano kushoto) akikagua miundombinu ya umeme katika Kata ya Kanyala wilayani Geita ambayo imepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III).Wa Tatu kulia ni Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyau na Wa Tano kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Josephat Maganga.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) katika Kijiji cha Lwezera wilayani Geita wakati alipofika kuwasha umeme katika Kijiji hicho.

No comments