Breaking News

PICHA:ZIARA YA MKUCHIKA WILAYANI LIWALE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bora Haule.

Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale wakimsikiliza Waziri George Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Luiza Mlelwa, akiwasilisha taarifa ya halmashauri yake kwa Waziri George Mkuchika.

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba akitoa utambulisho wa wageni waliohudhuria kikao kazi kati ya Waziri  George Mkuchika na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri hiyo mkoani Lindi.

No comments