Breaking News

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE


Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, John Magufuli amemteua Michael Wilfred Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Kabla ya uteuzihuo.  Ngumbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania – OUT).

Ng’umbi amechukua nafasi ya Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakatihuohuo, Rais Magufuli amemteua Jaji Stephen Mrimi Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT)

Jaji Magoiga amechukua nafasi ya Jaji Barke Mbaraka ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 19 Februari, 2019.


No comments