Breaking News

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU KUTOKEA NCHINI CHINA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akisalimiana na Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo na Miahipa ya fahamu Zhao Yuan kutoka Hospital ya kimataifa  ya chuo kikuu cha Peking cha Beijing nchini China mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu.


Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Daktari Zhao Yuan aliye ambatana na Mjumbe wake, pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mhimbili Lawrence Maseru na Mkurugenzi Mtendaji wa Moi Respicious Boniface, Ikulu Jijini Dar es salaaam.


Rais Magufuli katika picha ya pamoja na Zhao Yuan, kutokea kulia ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke watatu kutokea kulia, pamoja na Mkurugenz Mtendaji wa Moi Respicious Boniface. wengine katika picha ni Waziri Ummy Mwalimu, Balozi Zuhura Bundala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Lawrence Maseru.


Rais Magufuli akiagana na Daktari Zhao Yuan wanne kutoka kulia mara baada ya kumaliza kupiga picha ya kumbukumbu Ikulu Jijini Dar es salaam.


Rais Magufuli akimkabidhi zawadi ya kinyago Daktari Zhao Yuan mara baada ya mazungumzo yao., Wakwanza kulia ni balozi wa China hapa nchini Wang Ke.


Rais Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo na Daktari Zhao Yuan. (Picha zote na Ikulu.)

No comments