Breaking News

TAARIFA HIZI ZIPUUZWE, HAZIFAI KUTUMIWA NA UMMA


IDARA ya Mpiga chapa mkuu wa Serikali imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya sheria takribani 41 zilizo fanyiwa urekebu kwaajili ya kuchapishwa kama toleo la mwaka 2018 kuwa si sahihi na zipuuzwe, hazifai kutumiwa na Umma.

Sheria hizo zilitangazwa kupitia tangazo la Serikali namba 674 la tarehe 2 Novemba 2018.

Taarifa rasmi toka katika idara hiyo imeeleza kuwa nakala tete za sheria hizo zinazo endelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii ambazo zipo katika mfumo wa “Word” zimebeba maelezo yanayo ashiria kuwa zimetoka katika idara ya kupiga chapa ya Serikali jambo ambalo si sahihi.

“tunapenda kueleza Umma kuwa Idara ya kupiga chapa ya Serikali inaendelea na maandalizi ya kuchapisha sheria hizo katika utaratibu wa kisheria wa uchapaji wa nyaraka za Serikali na pindi zitakapokuwa tayari zitatolewa na kutumika kama inavyohitajika.”

Aidha idara imekemea vikali vitendo hivyo vya upotoshwaji wa Umma na haitafumbia macho, endapo watabainika waliohusika kusambaza sheria hizo kinyume na taratibu na kanuni za uchapaji pamoja na utoaji wa taarifa kwa Umma.

No comments