Breaking News

TANZIA:MSANII GODZILLA AFARIKI DUNIA.Na mwndishi wetu
Msanii Golden Mbunda maarufu kama Godzilla anayefanya muziki wa miondoko ya Hip Hop amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwao Salasala Jijini Dar, mwili umehifadhiwa Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Taarifa zilizotofikia kutoka kwa watu wa karibu na marehemu zinadai kuwa presha ya mwananmuziki huyo ilishuka ghafla na sukari kupanda jambo lililopelekea kifo chake.


Godzilla atakumbukwa kwa umahiri wake na utunzi a nyimbo nyingi zilizofanya vizuri katika tasnia ya burudani nchini huku akiwa ni mmoja kati ya wasanii mahiri sana wa kuimba mashahiri ya papo kwa hapo ‘Freestyle’

No comments