Breaking News

PICHA:MKUCHIKA AWAPONGEZA WANANCHI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAFWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika  akizungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri  George Mkuchika, kuzungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa (hawapo pichani).

Wakazi wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa wakimsikiliza Waziri George Mkuchika  (hayupo pichani) 

 Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini,  Selemani Bungara akiishukuru serikali kwa kuufikisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani kwake wakati wa mkutano kati ya Waziri George Mkuchika  na wanufaika wa TASAF.  

Mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule Mwanahamisi Ukwenda akishuhudia namna alivyonufaika na TASAF  Kushoto kwake ni mnufaika mwenzie  Atili Swalehe.

 
Waziri  George Mkuchika (kulia) akikagua mradi wa mbuzi unaomilikiwa na Hassan Charahani (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na wanufaika wa TASAF.


No comments