Breaking News

ZAHERA ALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI.


KOCHA mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, ameitupia lawama safu yake ya ushambuliaji kwa kushindwa kufunga goli na kuvuna alama tatu katika mchezo wao dhidi ya Simba uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika Zahera alisema wapinzani wao walikuwa bora lakini anaamini timu yake ingeweza kufanya vizuri kama wachezaji wake wangekuwa wabunifu kila walipopeleka mashambulizi langoni kwa Simba.

"Wenzetu wanatimu nzuri ushindi walioupata unaakisi ubora wao, sisi tulicheza vizuri eneo la kuzuia na katikati, lakini wachezaji wangu walikosa ubunifu hasa katika eneo la kushambulia hivyo mashambulizi yetu hayakuwa yakifika mwisho." amesema Zahera.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Simba Mbeligiji Patrick Ausems amesema amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake sababu wamecheza vizuri na kufanikisha lengo walilo jipangia.

"Lengo letu lilikuwa ni kupata alama tatu, kwasababu ulikuwa ni mchezo muhim, tumecheza vizuri na tumestahiri kushinda." amesema Ausems.

Baada ya mchezo huo Simba wamefanikiwa kuondoka na alama tatu na kufikisha jumla ya alama39 na kusogea mpaka nafasi ya tatu huku wakiwa na michezo nane mkononi dhidi ya kinala wa msimamo huo Yanga.

No comments