Breaking News

BODI YA WAKURUGENZI TANESCO YATEMBELEA ENEO LA MRADI WA KUFUA UMEME KWA NJIA YA MAJI KATIKA MTO MALAGALASI, KIGOMA

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi, Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Alexander Kyaruzi  pamoja na wajumbe wengine  wa Bodi hiyo wametembelea mkoa wa Kigoma kujionea miradi mbalimbali ya kuzalisha na kusafirisha umeme.

Ziara ya bodi hiyo ilianza eneo la Kidahwe kilomita chache kutoka Kigpoma mjini ambako patajengwa kituo kikubwa cha kupoza na kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400 kutoka Nyakanazi. Eneo hilo lina ukubwa wa Hekta 406, Meneja Mwandamizi wa  TANESCO anayeshughulikia miradi Mhandisi Emmanuel Manirabona ambaye anafuatana na wajumbe wa bodi hiyo amesema.
“Mipango yetu ya badaye ni kukiunga kituo hiki na  njia ya Msongo wa Kilovolti 400 inayotoka Mpanda  hivyo kufanya nchi yetu kuwa imeunganishwa na mtandao wa umeme wa Gridi kwa njia  za Msongo wa Kilovolti 400,” Alisema Mhandisi Manirabona na kuongeza,  eneo hilo pia linatarajiwa kujengwa njia ya Msongo wa Kilovolti 132 kutoka kituo cha Kufua umeme wa maji cha Malagalasi,  pamoja na njia za usafirishaji umeme zitaunganisha wilaya zote za Mkoa wa Kigoma na kituo hicho hivyo kufanya Mkoa wa Kigoma kuwa na umeme bora na wa uhakika wakati wote.
Bodi hiyo ya TANESCO ikiongozwea na mwenyekiti wake, Alexander Kyaruzi pia ilipata fursa ya kutembelea eneo la mradi wa umeme wa maji wa maporomoko yam to Malagarasi Mkoani Kigoma.
Akizungumzia mradi huo wa Malagalasi, Kyaruzi alisema nia  ya bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO kufika katika eneo hilo la Maporomoko ya Mto Malagalasi ni kuhakikisha kuwa TANESCO inafanya taratibu zote  ili kuwezesha Mradi huu kutekelezwa ambapo Matarajio ni kuwa  Mradi wa Kufua umeme, katika Mto Malagalasi  utaondoa tatizo la Upungufu wa umeme katika Mkoa wa Kigoma na hivyo kuondokana kabisa na  Matumizi ya  Majenereta ambayo yanatumia mafuta yenye gharama kubwa za uendeshaji.
 “ Pamoja na jitihada zanazoendelea za kutaka kuiunga Kigoma Katika Gridi ya Taifa , Kituo hiki cha kufua umeme cha Malagalasi kitaongeza kiasi cha Megawati 45 katika Gridi hivyo kufanya Mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika.

No comments