Breaking News

CCM DODOMA YAZINDUA MKAKATI WA KUIMARISHA MASHINA.

Na. EZEKIEL MTONYOLE,DODOMA
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Bashiru Alli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkakati wa kukomaza Demokrasi katika mkoa wa Dodoma unaolenga kukipa ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo za dola kwa maana ya uchaguzi wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Katibu wa CCM mkao wa Dodoma Jamila Yusuph, ameeleza hayo jijini hapa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo utakaofanyika Machi 23 mwaka huu jijini Dodoma ambao utakwenda pamoja na ugawaji wa vitendea kazi.
Jamila amesema,umuhimu wa mkakati huo wa kukomaza  demokrasia katika mkoa wa Dodoma, unalenga kufikia malengo  ya kutimiza ilani ya CCM kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho ya mwaka 1977 toleo la 2017, katika Ibara ya Tano ya katiba inachozungumzia malengo na madhumuni ya CCM.
“Ukiangalia kwenye katiba yetu kipengele kidogo cha kwanza kinazungumzia lengo na dhumuni kuu la CCM kushinda katika chaguzi za serikali za mitaa na chaguzi kuu kwa upande Tanzania bara na Zanzibar ili kuunda na kushika dola kwa maana ya kuunda na kushika serikali kuu na serikali za mitaa katika jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar,”amesema. 
Amesema, kukomaza demokrasia katika mkoa wa wetu maana yake ni kuzingatia vipengele, ikiwa ni pamoja na kuimarisha misingi ya uongozi bora, uwajibikaji kwa viongozi na wanachama, kulinda na kudumisha nidhamu ya wanachama, kuongeza kiwango cha ushiriki kwa wanachama katika shughuli za maendeleo, ulinzi na usalama katika maeneo yao, kulinda na kudumisha nidhamu ya wanachama.
Amesema mkakati huo utawezesha viongozi wao kujenga mahusiano mazuri baina ya viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa taasisi zingine na makundi mbalimbali katika meneo yao.
“Mkakati huu tunaotaka kuuanzisha utatuwezesha viongozi na watendaji wa CCM hasa wa ngazi ya mashina waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo hasa katika kushughulikia kero na changamoto za wananchi katika maeneo yao, kuwezesha ofisi za mashina na matawi kujiimarisha kiuchumi ili weze kutatua changamoto zilizopo.
Jamila amesisitiza kwamba mashina ndicho chombo kinachodhihirisha uwepo na uhai na nguvu ya chama, na kufafanua kuwa ndio daraja la mawasiliano baina ya chama na wananchi ambao ndio wanatoa lidhaa ya CCM kuendelea kuwa madarakani.
Jamila ametaja malengo kuwa ni kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo, kwa maana ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani lengo ni kumpa zawadi rais na hasa baada ya kuipa Dodoma makao makuu.
Amesema CCM imelenga kuweka msukumo hasa katika  ujenzi na ukarabati wa ofisi za chama katika ngazi za mashina na matawi na utawasaidia kuhakikisha kuwa maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na chama yanatekelezwa inavyopaswa na kwa wakati katika mkoa wa Dodoma.

No comments