Breaking News

MAJALIWA AZINDUA UPANUZI WA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. 

Baadhi ya waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua  awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimpokea mtoto  Claribel Mwakatumbula (1) kutoka kwa mama ya Delfina Audax wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto, Claribel Mwakatumbula (1) wakati   alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Ilham Ally wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Ilham amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Jackline Vicent aliyejifungua mtoto Lois Ladislaus  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alitembelea wodi ya wazazi kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa haospitali hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Binti Mfalme Zahra Aga Khan  (wapili kushoto) wakifungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi, 9, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto, Zaynab Chaula, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na   kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa,  (Agence Francaise de Developpment), Christian Yoka.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Binti Mfalme Zahra Aga Khan baada ya kufungua awamu ya pili ya hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Binti Mfalme Zahra  Aga Khan  wakati alipowasili Kwenye hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo, Machi 9, 2019. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments