Breaking News

PICHA:BAADHI YA MATUKIO YALIYOJILI IKULU LEO.


Rais wa Tanzania John Magufuli akimuapisha Balozi Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Ikulu Jijini Dar es salaam.


Rais Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Rais  Magufuli akimuapisha Balozi Yahya Simba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia. 


Rais Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mawaziri wawili, Balozi mmoja na kushuhudia uapishwaji wa Maofisa watano wa Jeshi la Polisi. 

Rais wa  Tanzania John Magufuli akisalimiana na Kamishna Benedict Michael Wakulyamba mara baada ya hafla ya uapisho kukamilika. 


Rais Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Makamishna watano kutoka jeshi la Polisi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi, pamoja na Balozi Yahya Simba mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya hafla ya Uapisho. 


Rais Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Maofisa Mbalimbali wa Jeshi kutoka Jeshi la Polisi mara baada ya hafla ya Uapisho wa viongozi mbalimbali.


Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma   na  Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Makamishna watano kutoka Jeshi la Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimuapisha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Leonard Paul Lwabuzala ambaye ameteuliwa kuwa kamishna wa kamisheni ya polisi Fedha na Lojistiki, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha zote na Ikulu.)

No comments