Breaking News

TAARIFA KWA WATANZANIA.MAKAMU wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, Uganda kushiriki Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13 Machi. 
Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huu. 
Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii itatolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 
Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia  Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbaro. 

Imetolewa na: 
Ofisi ya Makamu wa Rais 
Dar es salaam 
11/03/2019

No comments