Breaking News

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KUTOKA SHIRIKA LA UMEME TANESCO.


Na Mwandishi Wetu
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini Wilaya ya Tegeta kutokana na katizo la umeme lililotokana na hitilafu kwenye njia ya umeme ya TG5.

MAENEO YANAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Tegeta, Wazo, Mivumoni yote, Madale yote, baadhi ya maeneo ya Boko, Mbweni, Bunju yote na Mabwepande yote

Wataalamu na mafundi wanaendelea na kazi ili kurejesha huduma ya umeme katika hali yake ya kawaida.

Tutaendelea kuwapa taairfa kadiri kazi inavyofanyika.

No comments