Breaking News

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake Jijini Dodoma Machi 13, 2019 alipokutana naye na kufanya mazungumzo.


Waziri Angellah Kairuki akizungumza na balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke pamoja na wenyeji alioambatana nao wakati wa kikao cha mazungumzo  na Waziri Kairuki kuhusu masuala ya fursa za uwekezaji nchini.

Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akizungumza jambo kwa Waziri Angellah Kairuki alipomtembelea Ofisini kwake Machi 13, 2019 Jijini Dodoma.

Waziri Angellah Kairuki akizungumza jambo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke wakati wa kikao hicho.

Mwakilishi wa masuala ya Biashara Afrika Bw.Martin Kent akizungumza jambo kwa Waziri Angellah Kairuki (Hayupo pichani) wakati walipomtembelea katika Ofisi zake Dodoma.

Waziri Angellah Kairuki akiteta jambo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumza yao, kulia ni Beth Arthy aliyeambatana na balozi huyo.

Waziri Angellah Kairuki (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe alioongozana nao.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments