Breaking News

HOSPITALI YA WIILAYA YASABABISHA KERO KWA WANANCHI.

Na EZEKIEL NASHON, CHAMWINO.
WANANCHI wa kata ya Mlowa barabarani Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, wamesema licha ya hospitali ya wilaya ya Chamwino kutakiwa kujengwa kwenye kata yao, kama wenyeji wamekuwa hawapati  kipaumbele cha ajira  katika ujenzi wa hospital hiyo.
Wameyabainisha hayo wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Uvccm mkoa wa Dodoma, waliotembelea mradi huo ikiwa ni sehemu ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika wilaya ya Chamwino.
Wananchi hao, waliojitambulisha  Paulina Mapuga, na Magret Msagati, wamesema kuwa hawapati fursa ya kupata ajira katika mradi huo, vilevile wengi waliopata si wakazi wa kata hiyo, pia hata wakipata ujira wake ni mdogo sana ambao haukidhi mahitaji yao.
“Ni kweli tumepata fulsa ya hospitali ya wilaya kujengwa katika eneo letu tunaishukuru sana serikali, lakini wenyeji wa hapa hawapati ajira katika ujenzi huo hususa ni vijana wetu,”
“Hata sisi akina mama tunaopata vibarua katika ujenzi huo hatupati kipato kizuri kwa siku tunaripwa elfu mbili hadi elfu mbili mia tano, kwa wiki tunapata elfu kumi hadi kumi na mbili hizi hazitutoshi tutajikwamua vipi na umasikini kwa namna hii tunaomba tusaidiwe kwa hilo” alisema Paulina Mapuga.

Akikitolea ufafanuzi wa kero hizo kwa uongozi wa uvccm, diwani wa kata hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati wa ujenzi wa hospitali hiyo, Allani Matewa, amesema tatizo kubwa linalosababisha tatizo hilo ni mafundi wanaotekeleza mradi huo kutokuwa na uwezo kiuchumi na kutokana na matakwa ya mikataba ambayo hutolewa na serikali,
“Tatizo kubwa lipo katika mikataba hii na ukizingatia mafundui wanaotumia ni hawa tunaita lacal fundi ambao hawana uwezo katika maswala ya fedha hivyo ndio husababisha haya yote, ukimwambia hadi afike hadi hatua ya kumaliza msingi hawawezi mwisho hata  wao wanashindwa kujikidhi wenyewe” alisema Matewa.
Vilevile ametolea ufafanuzi kwanini wenyeji wameshindwa kupata nafasi katika mradi huo kuwa ni  hilo la mafundi kutokuwa na  uwezo kiuchumi kwahiyo wenyeji wakishindwa kupata ujira kwa mda mfupi wanaondoka, pia  hatuwezi kumpangia fundi watu wakumfanyia kazi.
Kutokana na hilo Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha kundi la vijana, Mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile, amewataka wananchi wa kata hiyo kuwa na imani na serikali yao kwani inafanya mambo mengi kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo.
Amesema hata hiyo kero itashughurikiwa  ili kwa wao kufikisha katika ngazi za juu, hivyo waendelee kuwa na subira wakati mambo  hayo yanafanyiwa kazi na wahusika.
Kwa upnde wake afisa mapokezi wa mradi huo Michael Samatwa alibainisha kuwa tatizo kubwa linaloikabili mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto ni tatizo kubwakatika mradi huo.
Hospitali hiyo ni moja ya hospitali zinazojengwa na serikali katika kila halmashauri za Wilaya kote nchini,ili kuhakikisha inaboresha huduma za afya katika kila mahali, na hospitali hiyo inajengwa katika eneo hilo baada ya makao makuu ya wilaya inatarajiwa kujengwa hospitali kubwa ya Uhuru.
                  

No comments