Breaking News

KAMATI YA MADINI YAFANYA SEMINA NA WAJUMBE WAKE.


Watendaji mbalimbali kutoka Taasisi zilizo chini ya  Wizara ya Nishati pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi hizo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyohusu Sekta ya Nishati.


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati iliyofanyika jijini Dodoma.Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa kuhusu Sekta ya Nishati katika Semina ya Wajumbe hao iliyofanyika jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja  (PBPA), Erasto Simon, akiwasilisha taarifa kuhusu Wakala huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati.

No comments