Breaking News

KAULI YA UVCCM KWA MAGUFULI BAADA YA KUFUNGUA MJI WA KISERIKALI DODOMA.


Na EZEKIEL NASHON,  KONGWA.

JUMUIYA ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM, mkoa wa Dodoma kwa kauli moja wameunga mkono na kumpongeza Rais John Magufuli kwa kitendo cha kuzindua Mji wa kiserikali katika eneo la Mtumba, ambapo ilikuwa historia ya mda mrefu.

 Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Billy Chidabwa, akiwa katika Mji mdogo wa Kibaigwa Wilayani Kongwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari Chidabwa amesema UVCCM, Mkoa wa Dodoma wanaunga mkono kwa asilimia mia moja kitendo cha Rais kuzindua Mji wa kiserikali  kwani ilikuwa ndoto ya mda mrefu ambayo imedumu kwa takribani miaka 47, lakini sasa imefanikiwa.

Aidha amesema ujio wa makao  makuu, unakuja na fulsa mbali mbali na amempongeza kwa kuona haja ya kuwapa ajira vijana waliokuwa wakifanya kazi katika majengo hayo, amesema kitendo cha kuhamishia makao makuu Dodoma kumetengeneza fulsa nyingi sana kwa vijana, ambao watafaidika na uwepo wa makao makuu ya nchi, Dodoma.

“Niongee wazi sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi tunaunga mkono kitendo alichokifanya Rais Dkt John Mgufuli kwani ni kitendo cha kijasili sana tunajua ndugu zangu hii ilikuwa ndoto ya mda mrefu kuhamia Dodoma lakini Rais wa  awamu  hii amefanikiwa  kwa hiyo sisi kama vijana tunaunga mkono  asilimia miamoja”,

“Ndugu zangu hili ni jambo kubwa sana tumeona wenyewe kwa macho yetu Mh, Rais katangaza fulsa za ajira kwa vijana waliokuwa wakifanya kazi katika majengo yale wameajiriwa zaidi ya vijana  elfu moja, nje ya hapo watumishi waliohamia Dodoma ni zaidi ya elf nane(8000) hawa watakuwa na mahitaji mbali mbalimbali mama lishe watafaidika na wamachinga pia” amesema Chidabwa.

Amesema wao kama umoja wa vijana hawatasita kuikosoa serikali pale inapotakiwa kukosolewa kwani lengo ni kuona kila mwananchi anapata haki yake, amesema watakosoa baada kujiridhisha kama kweli pana uhitaji wa kukosolewa wao kama UVCCM hawatasita kukosoa kwa maslahi ya nchi.

Amesema kuwepo kwa makao makuu Dodoma kutachechea hali ya uchumi kwa Mkoa wa Dodoma, vilevile kutachochea uboreshaji wa miondombinu mbalimbali kutokana kuwa na makao makuu ya nchi hapa Dodoma tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Amesema wao kama  UVCCM mkoa wa Dodoma wataendelea kuwa mawakili wazuri kwa kuisemia serikali katika mambo mazuri yanayoendelea kufanyika katika nchi yetu, ambayo ni makubwa haijawahi kutokea katika nchi hii.

Kwa  upande wake Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha vijana Mariam Ditopile, amesema zoezi la kuhamia Dodoma limekuwa la kihistoria na wameamua kuwa wa kwanza kumupongeza Rais wa serikali ya awamu ya tano kwa uamuzi huo kwani kwa Dodoma imeandika historia kubwa sana ndani na nje ya nchi.

“Ndugu zangu sisi kama vijana na mimi nni Mbunge ninayetokana na vijana tumeona tuwe wa kwanza kumpongeza Rais wetu kwa sababu hili ni jambo la kihistoria na limeandika historia kubwa ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu kwa tukio hili  kwa sababu ni nchi chache sana zilizothubutu kufanya hivi na  zikafanikiwa” amesema Mariam.

Vilevile amebainisha  kuwa wanaposema serikali imehamia Dodoma ina maana ni mkoa mzima wa Dodoma na sio Dodoma Mjini tu, pia wilaya zingine zitapewa fulsa ya kupokea baadhi ya taasisi  nyingine ambapo pia nao watakuwa wamepata nao fulsa katika maeneo yao.

Aidha  ameahidi kuwa bajeti yoyote itakayopelekwa bungeni kwa ajiri ya kujenga makao makuu yeye atakuwa wa kwanza kuipitisha na kuwa balozi kwa wengine ili waipitishe iwe na manufaa kwa wananchi hasa wa Mkoa wa Dodoma.No comments