Breaking News

KIJAJI AWAFUNDA WATENDAJI WAKE.


Na Furaha John,Dodoma

NAIBU waziri wa fedha na mipango, Dk Ashatu Kijaji 
amesema  Wizara hiyo inabeba jukumu kubwa la kuhakikisha utekelezaji wa bajeti ya serikali unakidhi matarajio ya wananchi hususani wale wa kipato cha chini na kuwataka watendaji wote wa wizara hiyo kujipanga ili kutekeleza jukumu hilo muhimu.

Kijaji ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango na kuwataka watendaji hao kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi.

Amewataka watendaji hao kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali na kuwataka kuacha kuwaonea wananchi wanyonge kwa kuwatoza kodi kubwa kuliko
wanavyostahili kulipa bali kila mwananchi alipe kodi kulingana na biashara yake.

“Nasisitiza kaimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na ufuatiliaji wa matumizi pamoja na tathmini ya mpango wa bajeti ili kuhakikisha rasilimali fedha zilizopo zinatumika kwa ufanisi.” Amesisitiza Kijaji.

Amesema, wanapaswa kutumia busara na hekima hususani pale wanaposhughulikia na maslahi ya watumishi na wananchi kwa ujumla, kama viongozi tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa Watumishi pamoja na wadau wa nje kuhusu ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo.

Katika hatuna nyingine amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali kuacha tabia ya kuwaonea wananchi wanyonge kwa kuwatoza kodi kubwa kuliko wanavyostahili kulipa bali walipe kodi kulingana na biashara yake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na mipango ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo, Doto James amesema mkutano huo ni kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/ 2019 na kupitia mwelekeo wa makadirio ya bajeti ya mwaka 2019/2020 ambayo itawasilishwa rasmi bungeni June 9 mwaka huu.

"Tuna wajibu wao kusimamia kwa weledi utekelezaji wa bajeti hiyo kwani hatua hiyo inalenga kuisaidia serikali kufikia malengo hatimaye kukidhi matarajio ya wananchi ya kupata huduma bora na
kuboresha maisha yao," amesema James.


No comments