Breaking News

KITUO CHA POLISI KILICHOJENGWA MIAKA 25 ILIYOPITA SASA KUFUNGULIWA.


Na EZEKIEL  NASHON,  BAHI.
Baada ya kukaa kwa miaka 25 bila kufaunguliwa Kituo  cha polisi kilichojengwa kwa nguvu za wananchi ambacho kipo  katika kijiji cha Chipanga A, kata ya Chipanga, Wilaya ya  Bahi Mkoani  Dodoma, kinatarajiwa kufunguliwa hizi karibuni baada ya kupangiwa askari.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omar Badweli, wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya  UVCCM, Mkoa wa Dodoma walipotembelea kata  hiyo ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama, na kuangalia ushiriki wa vijana katika shughuri za maendeleo.

Badweli, amesema kituo hicho kilijengwa miaka 25 iliyopita tangu akiwa diwani wa kata hiyo lakini hakijawahi kufunguliwa licha ya kuleta mawaziri na ma Rpc lakini hakijawahi kufunguliwa, lakini habari njema ni kwamba amepokea simu kutoka makao makuu ya polisi kuwa kituo hicho kimepangiwa askari.

Amesema tayari ameshaitisha mkutano wa tarafa nzima ili kupeana taarifa kuwa inabidi wakutane ili kukifanyia ukarabati kituo hicho ili kianze kufanya kazi.

“Mheshimiwa mgeni rasmi ni kweli kama walivyoongea wananchi shida ya kituo cha polisi ilikuwa kubwa kwa sababu ujenzi huu umejengwa miaka 25 iliyopita tangu nikiwa diwani wa kata hii, lakini habari njema ni kwamba nimepokea simu kutoka makao makuu ya polisi kuwa kituo kimepangiwa askari” alisema Badweli.

Kabla ya kauli hiyo mwenyekiti wa Chama cha  mapinduzi kata ya Chipanga, Yohana Chibagwa, kubainisha kuwa kituo hicho  kimejengwa kwa nguvu za wananchi miaka 25 iliyopita lakini mpaka sasa hakijafunguliwa hadi majengo yake yamechakaa.

Aidha kwa upande mwingine mwenyekiti alibainisha kuwa kijijini hapo kuna tatizo la maji kikwazo ni umeme wa kuendeshea mradi wa visima, chakushangaza ni kwamba umeme unaotarajiwa kuingia kijijini hapo nguzo hazijafika katika maradi  huo, hali itakayo sababisha tatizo la maji kuendelea kuwepo.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha kundi vijana, Mariam Ditopile, aliwahakikishia kuwa  umeme utafika hadi kwenye mradi wa maji, atatumia ushawishi wake kuhakikisha nguzo zinaingia katika mradi wa maji ili wananchi waweze kupata huduma ya maji  safi.

Amesema hali hiyo ndio iliyosababisha Rea awamu ya tatu mzunguko wa pili kuja kwa sababu waligundua kuwa ni kweli umeme unafika vijijini lakini hausambai au haugusi huduma za kijamii na kuruka baadhi ya vijiji hivyo mzunguko wa pili utakuja kutatua kero hizo.

“Niwahakikishie umeme utafika hadi kwenye mradi wa maji kwa sababu, hiyo ndio sababu ya Rea awamu tatu mzunguko wa pili, ili ukaguse vijiji vyote na kuingia kwenye miradi ya maendeleo, kwahiyo lazima umeme ufike kwenye mradi” alisema Mariam.

Katika kijiji hicho Mbunge Mariam Ditopile, pia alitoa mifuko 10 ya saruji kwa ajiri ya Zahanati ya kijiji, laki moja na nusu (150,000), kwa ajiri ya kuchangia upauaji wa darasa la shule ya msingi, laki na nusu (150,000) kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya walimu, na akatoa jezi seti mbili(2) na mpira miwili (2) kwa vijana ili kushiriki katika michezo, pia mbunge wa jimbo hilo alitoa mipira 3.

Kwa upande wake mkuu wa msafara wa kamati ya utekelezaji ya  UVCCM, Amani Mlagizi, alionya tabia ya viongozi kuwekana kwenye nafasi na kusababisha kudorola kwa maendeleo kutokana na kutokuwa na uelewa wa majukumu yao, waache na badala yake wachague  viongozi  kwa haki.

Pia alihimiza kwa wakuu wa mashina kukomaza demokrasia kwenye maeneo yao na kuhakikisha  chama  kinaibuka na ushindi katika ngazi zote ili chama kiendelee kushika dola.


No comments