Breaking News

MADRID YAPANIA KUNG'OA NGUZO ZA UNITED, CHELSEA.

Miamba ya Soka barani Ulaya Real Madrid, imeanzisha mkakati kabambe wa kumsajili kiungo tegemeo wa Manchester United, Mfaransa Paul Pogba.

Madrid wameupa  Jina rasmi mpango huo la ‘Operation Pogba’ na klabu hiyo itamng'oa Pogba mara tu baada ya kukamilisha usajili wa Eden Hazard , kwa mujibu wa taarifa kutoka Marca.

Real wanajiamini kuhusu kumnasa Hazard majira ya kiangazi na kwa haraka sana watahamishia nguvu zao katika kupata saini ya Pogba pindi Hazard akiwa ameshatua Bernabeu.

Wakala wa Pogba , Mino Raiola ameripotiwa kutaka kufanikisha uhamisho huo kwa mteja wake ambaye amemuambia kwamba anataka kucheza Real Madrid siku moja.

No comments