Breaking News

MAGUFULI AKAGUA MASHAMBA YA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO LA KITAI MBINGA.Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike mara baada ya kuwasili katika eneo la Mashamba ya Mahindi ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma.
 
Dkt. Magufulia akikagua Mashamba ya mahindi ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma huku akitoa maelekezo kwa viongozi hao wa Jeshi la Magereza nchini.
 
Sehemu ya Mashamba hayo ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma ambayo yamelimwa ekari 650 za mahindi katika mwaka huu.

 
Sehemu ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli aliyokuwa akiitoa katika eneohilo la Kitai Mbinga mkoa ni Ruvuma.
 
Dkt. Magufuli akizungumza na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza katika eneo la Gereza la Kitai  mara baada ya kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza hilo lililopo Mbinga mkoani Ruvuma.
 
Dkt. Magufuli akizungumza huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat Komba ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika  Shule ya Msingi ya Kitai. Ambapo Dkt. Magufuli alichangia kiasi cha Shilingi milioni tano kwaajili ya ujenzi wa vyoo.
 
Dkt. Magufuli akizungumza huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat Komba ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika   Shule ya Msingi ya Kitai. Wapili kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Onesmo Luwena
 
Dkt. Magufuli akisalimiana na wanafunzi wa  Shule ya Msingi ya Kitai mara baada ya kuwachangia kiasi cha Shilingi milioni tano.
 
Dkt. Magufuli akizungumza jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike mara baada ya kuwahutubia. PICHA NA IKULU


No comments