Breaking News

MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA , UJENZI WA BARABARA KM 107.4 MKOANI NJOMBE.Dkt. Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wengine  akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
 
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
 
Dkt. Magufuli akikagua maeneo mbalimbali ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambayo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho kukamilika.
 
Dkt. Magufuli akizungumza na wafanyakazi mbalimbali, pamoja na wakandarasi wanaojenga majengo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
 
Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wengine mara baada ya ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
 
Dkt. Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete km 107.4
 
Dkt. Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete km 107.4.
 
Dkt. Magufuli akiimba pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ramadhani wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete km 107.4.
 
Dkt. Magufuli akiangalia Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ramadhani walipokuwa wakimuonesha Shule yao ilipo pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete. Mkandarasi wa barabara hiyo amewaahidi watoto hao kuwajengea vyumba vya madarasa.
 
Dkt. Magufuli akizungumza na Wananchi waishio pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete mara baada ya kuiwekea jiwe la msingi.
 
Dkt. Magufuli akizungumza na Wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya sabasaba mkoani Njombe. 
 
Dkt. Magufuli akiwa pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo yaliokuwa yakitolewa na Dkt. Mkoni kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe kabla ya kuweka jiwe la msingi hospitalini hapo.
 
Dkt. Magufuli akiwapungiamkono pamoja na kuwashukuru wanachi wa Njombe waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba mkoani humo.
 
Dkt. Magufuli akiangalia jengo hilo la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
 
Baadhi ya wakazi wa Njombe wakiwa katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya sabasaba.


Sehemu ya jengo la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe. PICHA NA IKULU.


No comments