Breaking News

MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANAMIGORI AKIELEKEA DODOMA.


Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Migori katika jimbo la Isimani mkoani Iringa wakati akielekea mkoani Dodoma.


Dkt. Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Migori katika jimbo la Isimani mkoani Iringa wakati akielekea mkoani Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi pamoja na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakishangilia mara baada ya Dkt. Magufuli kuagiza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Shilingi milioni 400 katika eneo la Migori mkoani Iringa.Wananchi wa Migori wakishangilia mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuagiza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Shilingi milioni 400 katika eneo la Migori mkoani Iringa.
 
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa kuwashukuru wakati kabla ya kuelekea mkoani Dodoma.


Dkt. Magufuli akiagana na machhifu wa Kimila wa mkoa wa Iringa mara baada ya kuwashukuru viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa.
 
Dkt. Magufuli akizungumza huku akiwa ameshika Kitambulisho cha Mjasiriamali mdogo  (Mmachinga) ambae amedai kuwa bado wanatozwa ushuru. Dkt. Magufuli amepiga marufuku kudai ushuru kwa wafanyabiashara wote wenye vitambulisho hivyo ambao mtaji wao hauzidi Shilingi milioni 4. PICHA NA IKULU

No comments