Breaking News

ZIARA YA MWENYEKITI WA TUME YA MADINI IDRIS KIKULA MKOANI MOROGORO.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula, Kamishna wa Tume Dkt. Athanas Macheyeki na baadhi ya wafanyakazi wa Tume hiyo mkoa wa Morogoro wakitembelea maeneo mbalimbali kuzunguka ofisi za Tume hiyo mara baada ya kikao cha pamoja.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akiongea na wafanyakazi wa Tume ya Madini kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za Tume hiyo mkoani Morogoro. Kulia kwake ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali yaliyo wasilishwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi  Morogoro wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa Tume ya Madini alipotembelea kwa ziara ya kikazi. Kulia kwake ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki na kushoto ni Mhandisi Emmanuel Shija Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro.

Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija akisoma taarifa ya utekelezaji wa shuguli mbalimbali za Tume hiyo kwa mkoa wa Morogoro mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prfo. Kikula.

Dkt. Athanas Macheyeki Kamishna wa Tume ya Madini mwenye vitabu mkononi akimsikiliza jambo Mwenyekiti wa Tume Prof. Kikula wakati wakikagua maeneo mbalimbali yanayo zunguka ofisi za   Tume ya Madini Mkoa wa Morogoro.

No comments